HISTORIA YA WATUMISHI SINGERS.
SHUKRANI;
Tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa Bwana wetu Yesu
Kristo ,kanisa kwa ujumla kwa maombi yenu pamoja na wafadhili wetu
waliotufadhili kwa njia moja au nyingine. Mungu awabariki sana.
KUANZA KWA
KIKUNDI
Wazo hili la kuanzisha kikundi cha injili kwa njia ya uimbaji
lilitoka baina ya familia mbili ambazo ni familia ya Magita Mataro na Kasoga
Kasika mnamo mwaka 2015 na kushiriki katika huduma mbalimbali za kanisa kwa
nafasi zilizoweza kupatikana.
Ilipofika mwaka 2016 wazo liliwapendeza pia baadhi ya
marafiki katika familia hizi mbili na kuamua kujiunga ili kuitenda kazi kwa
nguvu zaidi. Mwezi septemba 2016 kikundi kilisajiliwa rasmi katika kanisa
kikiwa na jumla ya waimbaji saba. Zoezi la usajili wa waimbaji liliendelea
mpaka kufikia waimbaji 13.
MALENGO YA
KIKUNDI
Kikundi kilianzishwa kikiwa na malengo yafuatayo:-
·
Kufanya kazi ya injili kwa njia ya uimbaji, mikutano
ya injili na huduma mbalimbali za kijamii na kiroho pia.
·
Kufanya shughuli za ujasiriamali ili kupata kipata
kufanikisha malengo ya kikundi.
MAFANIKIO
·
Kwa kutumia michango yetu wenyewe tumefanikiwa
kurekodi santuri ya sauti (Audio CD) iliyotugharimu takribani shilingi
1,500,000/= yenye jina la KESHENI.
·
Tumefanikiwa kutembelea kwa kusudi injili na kuomba na
familia mbalimbali ndani na nje ya kanisa.
No comments:
Post a Comment